Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Reza Aref, amesisitiza umuhimu wa kuingiza masomo ya akili bandia (Artificial Intelligence – AI) na usalama wa mtandao katika mfumo wa elimu nchini humo.
Aref alisema kuwa uzoefu wa matukio ya hivi karibuni umeonyesha nafasi muhimu ya teknolojia za kisasa katika masuala ya usalama na maendeleo ya taifa, hivyo kuna haja ya wanafunzi kuandaliwa mapema kwa kuwapatia elimu ya vitendo na inayolenga kujenga ujuzi katika nyanja hizo.
Alibainisha kuwa ufundishaji wa akili bandia na usalama wa mtandao unapaswa kuzingatia mafunzo ya kiutendaji badala ya nadharia pekee, ili kuwajengea vijana uwezo wa kukabiliana na changamoto za teknolojia na mahitaji ya siku zijazo.
Kauli hiyo inaakisi msisitizo wa viongozi wa Iran juu ya kuimarisha uwezo wa kizazi kipya katika sekta za teknolojia za kisasa na usalama wa kidijitali.
Your Comment